Tanzania yapanda viwango vya FIFA

0
968

Tanzania imepanda kwa nafasi mbili katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kwa wanaume, kutoka nafasi ya 121 iliyokuwepo Desemba 2023 hadi nafasi ya 119 Februari 2024.

Kwa Afrika, Tanzania inashika nafasi ya 30, ikizidiwa na majirani zake wa Afrika Mashariki ambapo Kenya ipo nafasi ya 26 Afrika na 111 dunia, Uganda ipo nafasi ya 19 Afrika na 92 duniani.

Katika historia ya Tanzania, nafasi ya juu zaidi ambayo imewahi kufika ni nafasi ya 65 duniani Februari 1995, huku nafasi ya chini zaidi ikiwa ni 175 Oktoba 2005.