Timu ya Taifa ya Karate ya Tanzania imeng’ara katika mashindano ya kimataifa ya Karate kwa nchi za maziwa makuu yaliyofanyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kumalizika Oktoba 23.
“Kwa ujumla tumepata medali 27 kwa ‘categories’ tofauti tofauti ambapo wanawake wameleta medali 13 na wanaume medali 14,” alisema kiongozi wa Chama cha Karate nchini.
“Katika medali hizo tuna Gold 7, Silver 8 na Bronze 12,” ameongeza kocha huyo.
Timu hiyo iliondoka nchini kupitia Rwanda baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Michezo kukwamua changamoto ya usafiri na vibali kwa ajili ya Timu hiyo kuvuka kupitia mpaka wa Rwanda uliokuwa umefungwa.