Tanzania yafuzu AFCON 2021

0
196

Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Ufukweni imefuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa ushindi wa jumla wa mabao 12-9 dhidi ya Burundi.

Mchezo wa kwanza Tanzania iliibuka na ushindi wa mabao 8-3 na mchezo wa pili imefungwa magoli 6-4.

Fainali hizo zitachezwa nchini Senegal kuanzia Mei 23 hadi Mei 29 mwaka huu.

Mshindi wa kwanza na wa pili wataiwakilisha Afrika katika fainali za Kombe la Duniani la Soka la Ufukweni (FIFA Beach Soccer World Cup) itakayofanyika nchini Urusi mwaka huu.