Tanzania yafuzu AFCON 2019

0
466

Tanzania imefuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Misri mwezi Juni mwaka huu.

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kufuzu fainali hizo ikiwa imefanya hivyo pia mwaka 1980.

Tanzania imefuzu baada ya kuichapa Uganda mabao Matatu kwa Sifuri na kushika nafasi ya pili kwenye kundi L, ikifikisha pointi Nane nyuma ya vinara Uganda wenye pointi 13.

Mchezo huo umechezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.