Tanzania Prisons, Singida Big Stars zafungiwa usajili

0
960

Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imezifungia kusajili klabu mbili za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambazo ni Tanzania Prisons na Singida Big Stars, kwa kosa la kusajili wachezaji wenye mikataba na timu zingine.

Tanzania Prisons ilimsajili golikipa Musa Mbise wa Coastal Union ikifahamu kuwa bado ana mkataba na timu hiyo.

Nayo Singida Big Stars ilimsainisha kipa Metacha Mnata kutoka Polisi Tanzania akiwa bado ana mkataba na timu hiyo.

Kamati imezikumbusha klabu zote nchini kuwa usajili wa wachezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni, na klabu zinazokikuka hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.