Tanzania kutoshiriki Miss World 2021

0
2840

Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la urembo la dunia (Miss World)  kwa mwaka huu Juliana Rugumisa,  hatoweza kushiriki shindano hilo lililopangwa kufanyika tarehe 16 mwezi huu nchini Puerto Rico kutokana na kukosa Visa.

Waandaaji wa Miss Tanzania wameeleza kwamba kutokana na changamoto Ugonjwa wa Virusi Korona (UVIKO19) kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa viza

Taarifa hiyo imetolewa na uongozi wa Kamati ya Miss Tanzania kupitia mtandao wake wa Instagram.

“Kesho Tarehe 3 December 2021 ndio mwisho wa kuingia kambi ya Miss World baada ya nchi nyingi kupata changamoto ya kuchelewa kupata Visa ya Marekani kwa wakati. Miss World wakaongeza muda na kuruhusu hadi ikifika hiyo kesho iwe mwisho.” imeeleza taarifa hiyo.

Tayari Wawakilishi kutoka nchi mbalimbali duniani wameshawasili nchini Puerto Rico kushiriki shindano hilo kubwa la urembo duniani.

“Hii ndio kusema kwa mwaka huu haitawezekana tena, hata hivyo mwisho wa mashindano ndio mwanzo wa mashindano yajayo, tunashukuru sana wadau wetu Miss World kwa jitihada kubwa na kuhakikisha hadi tunapata appointment mapema badala ya Januari.“ imeongeza taarifa hiyo ya uongozi wa  Kamati ya Miss Tanzania