TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA SEKTA YA MICHEZO

0
498

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuimarisha sekta ya michezo kwa kuendeleza vipaji na kuwekeza kwenye uboreshaji wa viwanja katika hadhi ya kimataifa

Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ameyasema hayo leo wakati akifungua na kufunga Mkutano wa Baraza la Michezo kanda ya IV ngazi ya Mawaziri unaofanyika Jijini Arusha Tangu Mei 2 hadi leo Mei 4, 2023

Aidha Waziri Mkuu amesema matukio yote ya michezo nchini yanalenga kuimarisha sekta hiyo na kuwataka viongozi kusimamia vyema sekta hiyo ili kuendelea kupata medani nyingi zaidi na kuvutia utalii wa Tanzania

Wakati wa mkutano huo Rais Samia Suluhu Hassan alipata fursa ya kuzungumza na wajumbe wa mkutano huo kwa njia ya video na kuwataka kuitumia vyema fursa hiyo kuandaa michezo mbalimbali katika ukanda huu pamoja na kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania bara na Tanzania Zanzibar