Taifa Stars waendelea kujinoa kwa Afcon

0
557

Timu ya Taifa ya soka – Taifa Stars leo imeingia kwenye siku yake ya pili ya mazoezi, kujiandaa na michuano ya Afrika itayofanyika huko nchini Misri kuanzia June 21 mwaka huu.

Taifa Stars chini ya kocha wake Mkuu Emmanuel Amunike na msaidizi wake Hemed Moroco,  ilianza mazoezi jana Jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Karibu wachezaji wote wa Taifa Stars wamesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo,  wakiwemo wale wanaocheza soka nje ya nchi.

Taifa Stars itaweka kambi hapa nchini kwa muda wa wiki moja,  kabla ya kwenda nchini Misri ambako itaweka kambi ya wiki mbili na kucheza michezo miwili ya kirafiki,  kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ya Afrika.

Timu hiyo itacheza mchezo wa kirafiki na Misri June 13  mwaka huu na June 16 itacheza mchezo mwingine na Zimbabwe ama Nigeria.