Simba yapangwa kundi moja na Al Ahly, AS Vita Club na El Merreikh

0
239

Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imepangwa kwenye kundi A ikiwa na Mabingwa Watetezi Al Ahly, AS Vita Club pamoja na El Merreikh ya Sudan katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Droo ya upangaji wa makundi hayo imefanyika hii leo nchini Misri ambapo timu 16 zilizofuzu hatua ya makundi katika Ligi hiyo zimepangwa katika makundi manne.

Kila timu itacheza mechi sita, yani mechi tatu nyumbani na mechi tatu ugenini, na timu mbili zitakazoshika nafasi za juu ndizo zitakazoingia hatua ya robo fainali.