Simba yamsimamisha Morrison kwa utovu wa nidhamu

0
2073

Klabu ya Simba imemsimamisha kwa muda mchezaji Bernard Morrison hadi suala lake la kinidhamu litakapopatiwa ufumbuzi.

Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez, imesema Morrison amekuwa na tabia ya kutoka kambini bila ruhusa, kinyume na utaratibu.

Kufuatia kadhia hiyo Uongozi umemsimamisha kwa muda na kumtaka atoe maelezo ya maandishi kwa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba na akishindwa kufanya hivyo hatua zaidi za kinidhamu zitachukuliwa.