Simba yamkana Muharami

0
206

Klabu ya soka ya Simba imesema haihusiki na tuhuma zinazomkabili aliyewahi kuwa kocha wa magolikipa wa timu hiyo Muharami Said “Shilton”.

Hatua hiyo ya Simba inakuja muda mchache baada ya kamishna Jenerali wa Kupambana na kudhibiti dawa za kulevya nchini (DCEA) Gerald Kusaya kumtaja Mharami kuwa ni miongoni mwa watu 9 wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya zaidi ya kilo 34.9.

Taarifa ya Simba SC kupitia App yake imeeleza kuwa Muharami hakuwa na mkataba na klabu hiyo na kwamba walimuomba kwa muda wa mwezi mmoja asaidie kuwanoa walinda lango wa Klabu hiyo na muda wake uliisha.

Hata hivyo Simba wameeleza kuwa wapo tayari kutoa ushirikiano wowote unaohitajika kuhusiana na tuhuma hizo.