Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, -Simba wameshatua mjini Morogoro tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar ambao unatarajiwa kuwa wa kuvutia.
Meneja wa timu ya Simba,- Patrick Rweyemamu amesema kuwa, wapo kamili na watapambana ili waweze kushinda mchezo huo.
Simba inakutana na Mtibwa Sugar baada ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya JKT Tanzania kwa bao moja kwa bila huku Mtibwa Sugar wakifungwa na Lipuli FC kwa idadi hiyo hiyo ya bao moja kwa bila.
Mchezo mwingine wa kesho Yanga watakipiga na Mbeya City kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam majira ya saa Moja jioni.
Michezo yote hiyo itatangazwa moja kwa moja na TBC Taifa.