Klabu ya soka ya Simba imeondoka na alama tatu kutoka Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya wenyeji wao, Coastal Union FC kukubali kipigo cha magoli 2-1.
Simba ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli katika Dakika ya 40 kipindi cha kwanza kupitia kwa Benard Morrison, kabla ya Wagosi wa Kaya kusawazisha katika dakika ya 77 ya kipindi cha pili Kupitia kwa kiungo wake Raia wa Nigeria Victor Akpan kabla ya Mnyarwanda Meddie Kagere akarejesha furaha Msimbazi kwa kufunga goli la ushindi dakika za nyiongeza.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha alama 40, baada ya kucheza michezo 18 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimano wa ligi.
Aidha, Coastal Union imebaki nafasi ya 12 ikiwa na alama 21 baada ya kushuka dimbani mara 19.
Coastal Union wameendelea kuwa wateja wa Simba ambapo hawajashinda mchezo wowote tangu mwaka 2015.