Wekundu wa Msimbazi Simba wameibamiza ASEC Mimosas ya Ivory Coast mabao 3 kwa 1 katika mchezo wa kwanza wa kundi D wa kombe la shirikisho mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Mabao ya Simba yamefungwa na Pape Sakho dakika ya 13, Shomari Kapombe akifunga kwa mkwaju wa penalt dakika ya 79 na bao la 3 likifungwa na Peter Banda dakika ya 81
Bao lakufutia machozi kwa upande wa ASEC Mimosas limefungwa na Stephane Aziz Ki dakika ya 60 ya mchezo huo