Simba Queens yaanza kwa kishindo michuano ya Afrika

0
1968

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake, Simba Queens imeanza michuano hiyo kwa kishindo baada ya kuitandika PVP ya Burundi mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa katika Dimba la Nyayo jijini Nairobi.

Michuano hiyo ambayo inachezwa kwa kanda imefunguliwa hii leo ambapo katika mchezo wa ufunguzi Lady Doves ya Uganda imebuka na ushindi wa mabao 5- 0 dhidi ya FAD ya DJibout.

Simba Queens imepata mabao yake manne kupitia kwa Nyota wake Flavine Musolo aliyefunga mabao mawili, Aisha Mnunka na Danai Bhoho.