Simba na AL Ahaly uso kwa uso

0
777

Wawakilishi pekee katika michuano ya Kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika, –  Simba leo wanashuka dimbani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kucheza mchezo wa marudiano na AL Ahaly ya Misri .

Katika mchezo ambao Simba walikwenda ugenini nchini Misri,  walilala kwa magoli matano kwa bila huku wakiwa na kumbukumbu nyingine ya kufungwa magoli matano kutoka kwa AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Nahodha Msaidizi wa timu ya Simba, – Mohamed Hussein amesema kuwa kikosi chake kitatumia faida ya kucheza uwanja wa nyumbani ili kupata ushindi.

Simba inacheza mchezo huo ambao unaweza kuamua hatma ya kikosi hicho kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na ili kuendelea na michuano hiyo lazima ishinde.

AL Ahly ndiyo vinara wa kundi D wakiwa na alama Saba, wakifuatiwa na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wenye alama nne, Simba wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama tatu huku JS Saoura ya Algeria ikiburuza mkia baada ya kujikusanyia alama mbili.