Shindano la Miss World 2021 laahirishwa

0
2638

Shindano la Miss World 2021 limeahirishwa kwa muda wa siku 90, ambapo fainali ya kupata mshindi ilitarajiwa kufanyika leo 16 Desemba 2021 huko Puerto Rico.

Waandaji wa shindano hilo wametoa tamko la sababu ya maamuzi ikiwa ni masuala ya kiafya na usalama wa washindani, wafanyakazi na umma kwa ujumla.

Taarifa rasmi kwenye vyombo vya habari iliyotumwa mtandaoni na wasimamizi wa shindano la Miss World inasema baada ya kukutana na wataalam wa afya  na wataalam wa matibabu walioajiriwa kusimamia hafla ya Miss World 2021 na kujadili na Idara ya Afya ya Puerto Rico, wameahirisha shindano hilo na sasa litafanyika ndani ya siku 90 zijazo.

Kufikia jana, hatua za ziada za usalama zilitekelezwa kwa maslahi ya washindani, timu ya Miss world na watazamaji, tukio hilo liliongeza hatari kwenye jukwaa na katika chumba cha kubadilishia nguo.

Pia katika taarifa hiyo wasimamizi wa Miss world wamesema kumekuwa na ongezeko la visa vya UVIKO- 19 ambavyo vimethibitishwa asubuhi ya leo, na baada ya kushauriana na maafisa wa afya na wataalam, uamuzi wa kuahirishwa ulifanywa mara moja. Hatua hiyo imefuatana na kuwekwa karantini mara moja, ukisubiriwa uchunguzi na upimaji zaidi, na washiriki na wafanyikazi wanaohusika watarudi katika nchi zao baada ya karantini.

“Tunatazamia sana kurejea kwa washiriki wetu, (ambao tumekua tukiwafahamu na kuwapenda), kuwania taji la Miss World,” amesema Julia Morley, Mkurugenzi Mtendaji wa Miss World Ltd.

Katika shindano hilo Tanzania inawakilishwa na Juliana Rugumisa.