Sheria ya kupinga ubaguzi yapewa jina la Vini Jr

0
249

Sheria ya kupinga ubaguzi wa rangi imepewa jina la mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Jr.

Serikali ya Jiji la Rio de Janeiro nchini Brazil imesema ‘Sheria ya Vini Jr’, iliyoidhinishwa kwa kauli moja mwezi Juni itapelekea michezo kusimamishwa au kuahirishwa iwapo kutakuwa na vitendo vya kibaguzi.

Vinicius, mwenye umri wa miaka 22, alifanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi mara kadhaa msimu uliopita.

“Leo ni siku ya kipekee sana na natumai familia yangu iwe na fahari kubwa,” alisema katika hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Maracana, ambapo alifanya kwanza mechi yake ya kitaalamu na Flamengo.

“Nina umri mdogo sana na sikutarajia ningepokea heshima hii.”