Sasii ndiye hakimu Simba na Yanga

0
302

Herry Sasii ndiye atakayetafsiri sheria 17 za Mpira wa Miguu katika dakika 90 za Derby ya Kariakoo Desemba 11, 2021 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Sasii atasaidiwa na Kassim Mpanga na Hamdani Saidi.

Joto la mchezo huo limeanza kupanda ambapo mashabiki wa vilabu hivyo wanatambiana kuibuka na ushindi.

Mchezo wa mwisho kuzikutanisha timu hizo ni Ngao ya Jamii iliyopigwa Septemba 25 mwaka huu ambapo Yanga iliibuka na ushindi kwa goli la Fiston Mayele dakika ya 13.