Mashabiki wa soka wanashauku ya kutaka kujua uamuzi wa mwisho utakaotolewa leo kuhusu mvutano wa kimkataba kati ya Yanga SC dhidi ya Feisal Salum (Fei Toto).
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Said Sudi anatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho leo, lakini kukiwa na ruksa ya kukata rufaa kwa upande ambao hautaridhika na uamuzi huo.
Akizungumza mwishoni mwa mwiki alisema kuwa baada ya kupitia mkataba walijiridhisha kuwa Fei Toto bado ni mchezaji halali wa Yanga.
Hata hivyo wakili wa mchezaji huyo, Nduruma Majembe alisema kuwa haki haikutendeka na kwamba mteja wake hayuko tayari kurejea klabuni hapo.
Yanga inasisitiza kuwa kiungo huyo alikiuka makubaliano ya mkataba katika nia yake ya kutaka kuuvunja kabla ya mkataba huo kufikia mwisho mwaka 2024.