ROYAL TOUR YAIVUTA SOUTHAMPTON

0
189

Maafisa waandamizi wa masoko wa klabu soka ya Southampton FC ya nchini England wametua nchini tayari kufanya mazungumzo na serikali, ili kuona namna ya kuutangaza utalii wa Tanzania kwenye Ligi Kuu ya England.

Hapo kesho maafisa hao watakutana na kufanya mazungumzo na maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kufanikisha jambo hilo.

Ujio wa maafisa hao waandamizi wa masoko wa klabu soka ya Southampton ni moja ya mafanikio ya filamu ya Tanzania The Royal Tour iliyozinduliwa hivi karibuni, kwa lengo la kuutangaza utalii pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo nchini.