Ronaldo: Nasalitiwa United

0
179

Mambo yanaonekana kuwa si shwari ndani ya klabu ya Manchester United baada ya nyota wa klabu hiyo Christiano Ronaldo kutoa shutuma za kuhujumiwa.

Katika mahojiano yake na vyombo vya habari nchini Uingereza, Ronaldo amesema anahisi anahujumiwa ndani ya klabu hiyo.

“Nilitaka kwenda Manchester City lakini Sir Alex Ferguson (Kocha wa zamani wa Klabu hiyo) alinipigia na kuniambia sipaswi kwenda City nami sikutaka kumkatalia, nikaufuata moyo wangu na nikarejea Old Trafford.” amesema Ronaldo na kuongeza kuwa

“Nilidhani nitaona vitu tofauti ndani ya United lakini nimeshangaa mambo mengi ni yale yale tangu nilipokuwa nina miaka 20,21,22 teknolojia imebadilika ila United tupo pale pale”.

Amesema anahisi kusalitiwa na Man United na kwamba kuna baadhi ya watu hawataki awepo hapo na sio msimu huu tu ni tangu msimu uliopita wanataka aondoke.

“Sina heshima yoyote kwa Erik Ten Haag kwa kuwa yeye haniheshimu, kama wanataka kufanya mabadiliko ikiwemo kuniondosha ni sawa ila wanapaswa kubadili vitu vingi sana ndani ya United.” amesema Ronaldo