Ronaldo kumlipa mpenzi wake mamilioni ya fedha

0
299

Mitandao ya michezo imeripoti kuwa Cristiano Ronaldo amesaini makubaliano ya kabla ya ndoa (pre-nup agreement) ambapo imeelezwa kama ikitokea wakaachana, nyota huyo wa soka kutoka Ureno atakuwa akimlipa mpenzi wake Georgina Rodriguez Pauni 100,000 (zaidi ya shilingi Milioni 257) kila mwezi katika kipindi chote cha maisha yake.

Ronaldo na Georgina wana watoto wawili pamoja huku wakilea familia ya watoto watano ambao watatu Ronaldo aliwapata nje.