Ronaldo azidi kucheka na nyavu Italia

0
392

Cristiano Ronaldo amefunga penati yenye utata katika dakika za mwisho na kuiokoa Juventus na kipigo katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Italia dhidi ya AC Milan katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Juve walikuwa wanaelekea kupoteza mchezo wa tatu mfululizo ugenini baada ya Ante Rebic kuitanguliza AC Milan kwa kuifungia bao katika dakika ya 61 na dakika 10 baadae Milan wakapata pigo kwa mlinzi wake Theo Hernandez kutolewa nje kwa kadi nyekundu na katika dakika ya 90 VAR ikaipa Juve mkwaju wa penati uliokwamishwa wavuni na Ronaldo.

Bao alilofunga Ronaldo linamfanya kufunga katika michezo yote nane aliyocheza kwa mwaka huu wa 2020 na ni bao lake la 35 katika michezo 35 aliyoichezea timu yake ya taifa ya Ureno na timu yake ya Juventus.

Mchezo wa marudiano utachezwa Machi 4 mjini Turin.