Ronaldo afikisha mabao 125

0
598

Cristano Ronaldo amefikisha jumla ya mabao 125 ya kufunga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya usiku wa Aprili 10 mwaka huu kufunga bao katika sare ya bao moja kwa moja waliyoipata Juventus dhidi ya Ajax.

Katika mchezo huo wa robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, Ronaldo aliifungia Juve bao la kuongoza katika dakika ya 45 kabla ya David Neres kuisawazishia Juventus katika dakika ya 46.

Ronaldo sasa amefikisha mabao 598 ya kufunga kwenye maisha yake ya soka,  akibakiza mabao mawili kufikisha mabao 600 huku mpinzani wake mkubwa Lionel Messi akiwa amefunga mabao 594 mpaka sasa.

Katika mchezo mwingine wa robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya uliochezwa usiku wa Aprili 10 mwaka huu, Manchester United wakiwa nyumbani wamekubali kipigo cha bao moja kwa bila kutoka kwa FC Barcelona.

Mlinzi Luke Sho alijifunga katika dakika ya 12 kufuatia mpira wa kichwa uliopigwa na Luis Suares na kuipa Barca ushindi huo muhimu wa ugenini.

Kwingineko,  michezo Minne ya robo fainali ya michuano ya Yuropa inachezwa usiku wa leo ambapo Arsenal watakuwa nyumbani kuwaalika Napoli wakati Chelsea wakisafiri kuwafuata Slavia Prague huku Benefika wakiwakaribisha Entrancht Frankfurt na Villareal watakuwa wenyeji wa Valencia.