Klabu ya RB Leipzig imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mechi ya robo fainali uliopigwa kwenye dimba la Estadio Jose Alvalade nchini Ureno.
Magoli ya RB Leipzig yalifungwa na Daniel Olmo dakika ya 50 na Tyler Adams dakika ya 88 huku goli pekee la Atletico Madrid likitiwa kimiani na Joao Felix kwa mkwaju wa penati dakika ya 71.
Katika mchezo wa hatua inayofata ya nusu fainali ya michuano hiyo klabu ya RB Leipzig itakutana na Paris Saint-Germain mchezo ambao utapigwa Agosti 18, 2020.