Ramsey asajiliwa Juve

0
694

Kiungo wa klabu ya Arsenal ya nchini England, -Aaron Ramsey amesajiliwa na klabu ya Juventus ya nchini Italia kwa mkataba wa miaka minne,  akiwa mchezaji huru kutokana na mkataba wake ndani ya Arsenal kumalizika June 30 mwaka huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atajiunga na Juve Julai Mosi mwaka huu mara baada ya mkataba wake kumaliza, hivyo Arsenal imemtoa bure kutokana na mkataba kumalizika.

Ramsey atalipwa Paundi Laki Nne kwa wiki baada ya makubaliano hayo ya kujiunga na Juve msimu wa joto.

Ramsey alijiunga na Arsenal akitokea Cardiff City nayo ya nchini England  mwaka 2008 kwa kitita cha Paundi Milioni  Nne Nukta Nane ambapo pia alikua na mazungumzo na klabu ya Barcelona ya Hispania na PSG ya Ufaransa .