PSG yaadhimisha mwaka mpya wa China

0
466

Klabu ya PSG ya nchini Ufaransa imeendelea na utamaduni wake wa kuitambua jamii ya Wachina kwa kuvaa jezi maalum katika kuadhimisha mwaka Mpya wa Jadi China (Mwaka wa Sungura) kwenye mchezo wao dhidi ya Reims.

Majina katika jezi za wachezaji yameandikwa kwa lugha ya Mandarin, utamaduni ambao unatokana na klabu hiyo kuwa na washirika kutoka China ikiwa ni pamoja na Mengniu na PingAn.