Timu ya Paris Saint-Germain imeibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Rennes katika mchezo wa Super Cup kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Ufaransa.
Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Shenzhen Universiade Sports Centre nchini China, PSG walikuwa nyuma kwa bao moja bila hadi kipindi cha pili, mabadiliko yaliyofanywa na kocha Thomas Tuchel yakaipa nguvu timu hiyo na kurudisha bao hilo dakika ya 57 kupitia kwa Kylian Mbape na kuongeza bao la pili dakika ya 73 kupitia kwa mchezaji Angel Di Maria