Pienar kuendesha programu za michezo nchini

0
1031

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Everton ya England, – Steven Pienar anatarajiwa kuendesha programu maalumu za michezo kwa timu za vijana za mpira wa miguu nchini.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania, –  Tarimba Abbas  amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa Pienar atakuwepo nchini wakati wa michuano ya kombe la SportPesa ambapo ataitumia fursa hiyo kuendesha programu hizo ikiwemo kufanya mazoezi na timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Akizungumzia mashindano hayo ya kombe la SportPesa ya mwaka huu, Tarimba amesema kuwa ili kuendana na ushindani unaoonyeshwa na timu kutoka nchini Kenya, wameamua kuendesha mashindano hayo katikati ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara ili kuzipa nafasi timu za Tanzania kuonyesha ushindani.

Nao viongozi wa Mashirikisho ya nchi zinazotoa timu shiriki kwenye mashindano hayo wamezitaka timu zao kuonyesha ushindani.

Mashindano hayo ya kombe la SportPesa yanaanza kutimu vumbi Jumanne Januari 21 ambapo timu Nane kutoka Tanzania na Kenya zitachuana.