Picha ya Messi yavunja rekodi Instagram

0
263

Baada ya nguli wa mpira wa miguu Lionel Messi kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia ya kucheza mpira wa miguu, historia nyingine mpya imewekwa huko Instagram.

Nyota huyo wa soka wa Argentina alichapisha picha zake akiwa ameshikilia Kombe la Dunia kwenye ukurasa wake wa Instagram, chapisho ambalo kwa sasa linashika rekodi ya chapisho lililopendwa zaidi ‘most liked Instagram post’.

Katika muda wa saa 48 tangu lichapishwe, lilikuwa na ‘likes’ milioni 62 na hadi sasa lina zaidi ya likes milioni 68.2.

Kabla ya picha ya Messi kuchukua rekodi hiyo, picha iliyokuwa ikishika nafasi hiyo tangu 2019 ni picha ya yai ambayo ndiyo picha pekee kwenye akaunti ya @world_record_egg