Orlando Magic yaigaragaza Huston Rockets

0
692

Huston Rockets wakiwa ugenini wamekubali kichapo cha alama 126 kwa 106 kutoka kwa Orlando Magic, kwenye Ligi Kuu ya kulipwa ya mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA).

James Harden na Russel Westbrook kwa pamoja wamefunga alama 47,  lakini bado hazikutosha kuwapa Rockets ushindi mbele ya Magic waliokuwa wakiongozwa na Aaron Gordon aliyefunga alama 19.

Katika matokeo mengine, Washington Wizards wametandikwa alama mia moja  kwa 89 na Miami Heat wakati Indiana Pecers wakipata ushindi wa alama 112 kwa 109 dhidi ya Dallas Mavericks huku Clevaland Cavaliers wakiinyuka San Antonio Spurs alama 132 kwa 129 na New York Knicks wakiifunga Detroit Pistons alama 96 kwa 84.