Nusu fainali ya Mapinduzi Cup kuikutanisha miamba ya Tanzania Bara

0
526

Azam FC imetinga hatua ya Nusu Fainali ya Mapinduzi Cup baada ya kuwaadhibu mabarobaro wa Zanzibar, Yosso Boys kwa magoli 5-1.

Kufuatia ushindi huo, Azam itakutana na Yanga SC katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa saa 10:15 jioni katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Nusu fainali ya pili itazikutanisha Simba SC na Namungo FC, mchezo utakaonza saa 2:15 usiku katika uwanja huo huo.

Watakaoibuka na ushindi kwenye michezo hiyo itakayoikutanisha miamba ya soka kutoka Tanzania Bara, watakutana katika mchezo wa fainali utakaopigwa Januari 13.

Mashindano ya Mapinduzi Cup hufanyika kila mwaka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 58.

Yanga ndiyo mtetezi wa kombe hilo ililolitwaa mwaka 2021 baada ya kuifunga Simba jumla wa Penalti 4-3 baada ya kwenda suluhu katika dakika 90.