Neymar kukaa nje hadi mwisho wa msimu

0
279

Nyota wa PSG na Brazil, Neymar Jr huenda akawa nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu kutokana na kuhitaji kufanyiwa upasuaji katika kifundo cha mguu alikopata majeraha.

Neymar alipata majeraha hayo katika mchezo ambao waliibuka na ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya Lille katika uwanja wa nyumbani.

Klabu yake imesema kuwa amekuwa akipata majeraha ya mara kwa mara kwenye eneo hilo, hivyo anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuepusha hatari kubwa zaidi mbeleni.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu, matibabu hayo yatachukua miezi mitatu hadi minne.

Kutokana na majeraha ya kufundo cha mguu wa kulia, Neymar alikosa michezo miwili ya Brazil katika Kombe la Dunia mwaka 2022.