Timu ya Real Madrid imetinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya sare ya bila kufungana dhidi ya wenyeji, Liverpool usiku wa jana katika Uwanja wa Anfield.
Madrid inasonga mbele kwa ushindi wa 3-1 iliyovuna kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Hispania na sasa watakutana kwenye nusu fainali na Chelsea ya England iliyoitoa FC Porto ya Ureno katika hatua ya robo fainali
Manchester City wao wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 baada ya kushinda 2-1 kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita katika dimba la Etihad na sasa watakutana na PSG ya Ufaransa iliyowatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Bayern Munich.