Wakata miwa wa Manungu mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar FC wamefanikiwa kuwabana mbavu mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania, Simba SC na kutoka suluhu ya bila kufungana.
Mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wa Simba wakiamini timu yao itawapa furaha umepigwa katika Uwanja wa Manungu Complex, ukiwa ni mchezo wa kwanza baada ya uwanja huo kufunguliwa baada ya matengenezo.
Kwa matokeo hayo, Simba inazidi kuongeza utofauti wa alama kati yake na vinara wa ligi, Yanga SC, ambapo (Simba) imebakia nafasi ya pili ikiwa na alama 25 huku Mtibwa Sugar FC ikiwa nafasi ya 13 ikiwa na alama 12.
Timu hizo zitakutana tena Juni 12 mwaka huu katika mzunguko wa pili wa ligi, ambapo Simba watakuwa wenyeji.