Msuva Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora El Jadida

0
495

Simon Msuva ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2019 wa klabu ya Difaa El Jadida inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Msuva amepewa tuzo hiyo kwenye hafla iliyofanyika na kuandaliwa na Klabu hiyo

“Nimechukua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2019 ndani ya klabu yangu ya Difaa El Jadida si ligi. (tuzo zinazoandaliwa na klabu) mimi ndiye nimeshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu,” Simon Msuva.