Msimu mpya wa NBA mbioni kuanza

0
1311

Michezo miwili ya kirafiki ya mpira wa kikapu imechezwa nchini  Marekani ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya kulipwa ya mpira huo NBA.

Kwenye dimba la Toyota mjini Huston Texas,  wenyeji Huston Rockets wameshindwa kutamba baada ya kulazwa na Indiana Pecers alama 110 kwa 100 katika mchezo uliokuwa na ufundi mwingi huku matumizi ya nguvu pia yakichukua nafasi kubwa.

Victor Iladipo na Domantas Sabonis kwa pamoja wamefunga alama 39 na kucheza mipira iliyorudi yaani Rebounds 16 na kuchagiza ushindi huo wa ugenini mbele ya Rockets,  ushindi unaowapa mashabiki wa Pecers jeuri ya kufanya vyema kwenye msimu ujao wa NBA.

Licha ya James Harden kupambana na kufunga alama 18 na Brandon Ingram kufunga alama 19 na kucheza Rebounds tisa, bado hazikutosha kuwapa Rockets ushindi wakiwa nyumbani, hali iliyoibua hisia tofauti kwa mashabiki wa timu hiyo kuelekea msimu mpya wa ligi hiyo.

Mchezo wa mwisho wa kujipima ubavu umewakutanisha Los Angeles Lakers ambao wakiwa nyumbani Staples Center  mjini Los Angele-California,  wameibuka wababe kwa kuwanyuka Sacramento Kings alama 129 kwa 123.

Nyota mpya wa Lakers, -Lebron James ametakata kwa kufunga alama 18 na kucheza Rebounds tatu huku Brandon Ingram akiibuka nyota wa mchezo kwa kufunga alama 31 na kucheza Rebounds tisa wakati Kyle Kuzma na Josh Hart kila mmoja akifunga alama 17 kwa Lakers.

Licha ya Marvin Bargley, Dearon Fox na Budy Hield kufunga alama 53, bado hazikutosha kuwapa Kings ushindi katika mchezo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa.