Msimamo wa Qatar kuhusu pombe

0
218

Serikali ya Qatar imeitaka kampuni ya Budweiser ambayo ni wadhamini wa michuano ya Kombe la FIFA la Dunia itakayoanza nchini humo tarehe 20 mwezi huu, kuhamisha maduka yake ya pombe ambayo imeyaweka nje ya viwanja vyote vitakavyotumika kwenye michuano hiyo.

Qatar imeitaka kampuni hiyo kuhakikisha maduka hayo hayaonekani wazi, maana pombe sio kitu muhimu kwenye michuano hiyo.

Waandaji hao wamesema pombe itanywewa kwa mpangilio maalum na sio kila mahali kutokana na sheria za nchi hiyo.