Mshindi Bunge Marathon kubeba Mil.5

0
396

Mwenyekiti wa Bunge Marathon ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Makete mkoani Njombe, Festo Sanga amesema washindi wa mbio ndefu (Bunge Marathon) ambao ni mshindi wa mbio za kilomita 21 ataibuka na kitita cha shilingi Milioni tano, mshindi wa mbio za kilomita 10 shilingi Milioni tano na mshindi wa kilomita tano atabeba shilingi Milioni 1.5.

Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Aprili 13, 2024 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na ili kushiriki unapaswa kujisajili katika tovuti ya Bunge ambayo ni; marathon.bunge.go.tz

Sanga amewasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo zenye ada nafuu ya shilingi elfu 40, zinazolenga kuchangia ujenzi wa Shule ya sekondari ya Wavulana ya Bunge itakayojengwa jijini Dodoma.

Washiriki wa mbio hizo watapewa nafasi ya kuchagua wakimbie na nani kati ya Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Naibu Spika wa Bunge, Mawaziri au Mbunge wake.

#BungeMarathon #TBCupdates #TBCdigital