Mo Dewji ajiuzulu uongozi Simba

0
543

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo) ametangaza kujiuzulu wadhifa huo na kusema atabakia kama muwekezaji tu ndani ya klabu hiyo.
Katika ukurasa wake wa Twitter Mo ameandika kwa masikitiko makubwa kuwa kukosa ushindi kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi kumemfanya aachie ngazi huku akionesha kutoridhishwa na viwango vilivyoneshwa na wachezaji wake licha ya kulipa mishahara takribani shilingi bilioni 4 kwa mwaka.
Akiwa muwekezaji amesema atajikita kwenye maendeleo ya miundombinu na mafunzo ya soka kwa vijana.