Mkataba wa kwanza na Yanga ulikuwa mbovu

0
2016

“Mkataba wangu wa kwanza Yanga haukuwa mzuri nilikuwa hata siwezi kuondoka. Nilikuwa sijui Kiingereza, meneja wangu naye hajui Kiingereza anacheka cheka tu na viongozi, mkataba ulikuwa mgumu, mimi nimesaini tu nicheze nionekane,” amesema Fiston Mayele akizungumza na Azam TV.

Ameongeza kuwa “baada ya kucheza msimu wa kwanza kuna timu ilikuja inanitaka, nikawaambia mimi siondoki natakiwa kucheza msimu wa pili, wakaniambia utaongeza mkataba mwingine, nikawaambia sawa lakini nakuja na meneja mpya sio yule wa kucheka cheka hovyo.”

Amesema baada ya kumpata meneja mpya, Yasmin, mkataba unaoisha akashtuka namna ulivyokuwa, kisha akamsaidia kubadilisha akasaini mkataba mpya.