Misri kutumia viwanja Sita AFCON

0
821

Misri imepanga kutumia viwanja Sita vilivyopo katika miji mitano kwenye michuano ya mwaka huu ya Mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo itashirikisha jumla ya timu 24.

Moja ya viwanja vitakavyotumika kwa michuano hiyo ni ule wa Kimataifa wa Cairo pamoja na uwanja wa Port Said ambao mwaka 2012 kulitokea majanga yaliyosabisha vifo vya mashabiki 72 wa timu kongwe ya Al Ahly.

Baada ya tukio hilo uwanja huo ulifungwa na kufunguliwa tena mwaka 2018.

Viwanja hivyo vimeteuliwa na Chama Cha Soka Cha Misri (EFA) na viwanja vingine ni Alexandria, uwanja wa Ismailia, uwanja wa Suez na  uwanja wa Air Force.

Uwanja wa Kimataifa wa Cairo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki Elfu 75 umeshawahi kutumika kwenye michuano hiyo ya Afrika ya kwenye miaka ya 1974,1986 na 2006 ambayo Misri waliandaa na hii itakuwa ni mara yake ya nne kutumika kwa michuano hiyo mikubwa Barani Afrika.

Msemaji wa Chama Cha Soka Cha Misri, -Ahmed Megahed amesema kuwa awali walipendekeza viwanja nane kwa ajili ya kutumika kwenye michuano hiyo ya AFCON  ya mwaka huu,  lakini baadaye CAF ikaamua kuruhusu viwanja hivyo Sita pekee.