Miquissone avunja mkataba na Al Ahly

0
345

Klabu ya Al Ahly ya Misri imevunja mkataba na kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luís Jose Miquissone kwa makubaliano ya pande zote.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Miquissone kurejea kutoka Abha FC ya Saudi Arabia alikopelekwa kwa mkopo.

Kiungo huyo alijiunga na Al Ahly miaka miwili iliyopita akitokea Simba SC ya Tanzania, ambapo pia amewahi kucheza ligi za Msumbiji na Afrika Kusini.

Miquissone amekuwa akihusishwa na kurejea Simba SC, aliyoitumikia tangu aliposajiliwa mwaka 2020 akitokea UD Songo ya nchini Msumbiji na alikuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio ya Simba akiwa ameifungia magoli tisa na kutoa usaidizi wa magoli 15.