Michelle Alozie, mtaalam wa biolojia aliyegeukia soka Nigeria

0
364

Michelle Chikwendu Alozie, mzaliwa wa Marekani mwenye asili ya Nigeria amekuwa gumzo kwa namna ambavyo ameendelea kuweka uzani (balance) kwenye ndoto yake ya kuwa mwanasoka na kufanyakazi yake.

Alozie ambaye anacheza kama mlinzi kwenye timu ya wanawake ya Nigeria, Super Falcon, ni mhitimu wa shadaha ya biolojia (Molecular Biology) kutoka Chuo Kikuu cha Yale, Marekani na ambapo pamoja na kufanya kazi lakini anaweza kuendeleza ndoto yake ya kucheza mpira.

Mwanasoka huyo alizaliwa Aprili 28, 1997 ambapo mbali na kuwa mchezaji wa klabu ya Houston Dash inayoshiriki ligi ya wanawake nchini Marekani, pia hufanya kazi kama mtaalamu wa utafiti wa saratani katika Hospitali ya Watoto Texas.

Mwaka 2021 aliitwa kwa mara ya kwanza kwenye timu ya Taifa na kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Jamaica, na mwaka huu amejumuishwa kwenye kikosi kilichoshiriki Kombe la Dunia kwa Wanawake.

Nigeria imetolewa kwenye mashindano hayo kwa penati 4-2 dhidi ya England baada ya timu zote kutoka suluhu.