Nahodha wa Argentinal Lionel Messi amesema mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia 2022 ni mchezo wake wa mwisho wa Kombe la Dunia akiichezea Argentina.
Messi ambaye ameiwezesha Argetina kufuzu fainali baada ya kuifunga Croatia 3-0 haya ni mashindano yake ya tano akiwa na Argentina lakini hajawahi kutwaa taji hilo.
“Kuna miaka mingi kutoka sasa hadi kombe la dunia lijalo. Sidhani kama nitaweza kushiriki. Kufikia mwisho kwa namna hii ni fahari sana,” amesema.
Katika mchezo huo ambao Messi analenga kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza ataweka rekodi ya kuwa mcheza soka wa kiume aliyecheza mechi nyingi za Kombe la Dunia, ambapo atacheza mchezo wa 26.
Juni 2016 Messi alitangaza kustaafu soka la kimataifa, lakini alibadili uamuzi miezi miwili baadaye.
Messi anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa Argentina kufunga katika fainali nne za kombe la dunia, huku akiwa mfungaji bora wa muda wote wa mshindano hayo kwa nchi yake akiwa na magoli 11.