Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Lionel Messi, ameiambia klabu hiyo kuwa anataka kuondoka kutafuta maisha mengine, huku Manchester City ikiwa ni timu pekee inayoonesha shauku ya kutaka kumsajili.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Esporte Interativo’ wa Hispania Messi, 33, anashinikiza kuondoka kutokana na matokeo mabaya yanayoikumba timu hiyo.
Barcelona imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupokea kichapo cha mabao 8-2 kutoka kwa Bayern Munchen.
Nyota huyo wa Argentina anayeaminika kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya mchezo wa soka, ametumia muda wake wote akiwa na klabu hiyo yenye makao makuu yake Camp Nou kwa zaidi ya miaka kumi.