Mchezaji nyota wa klabu ya soka ya Barcelona ya Hispania, Lionel Messi ameanza mchakato wa kumtoa rumande mchezaji nyota wa zamani wa Brazil na Barcelona, Ronaldinho Gaucho.
Messi anatarajia kuwalipa mawakili Euro milioni 4 sawa na shilingi bilioni 10.5 ili kufanikisha kumtoa rumande nyota huyo wa kibrazil ambaye anashikiliwa nchini Paraguay kwa kosa la kughushi hati ya kusafiria.