Mchakato wa kutafuta kocha Azam waendelea

0
750

Klabu ya Azam imesema ipo katika mchakato wa kuhakikisha anapatikana kocha wa kukinoa kikosi hicho baada ya kumtimu kocha Hans Van Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi kutokana na mwenendo mbaya wa timu.

Msemaji wa Azam, – Jaffar Idd amesema kuwa kwa sasa wakiwa wanaendelea na kazi ya kutafuta kocha,  timu hiyo ipo chini ya makocha Meja Abdul Mingange na Idd Cheche.

Mtihani wao wa kwanza ni katika mchezo wa Kombe la Shirikisho ambapo Azam inashuka dimbani kucheza na Rhano Range ya mkoani Tabora.

Makocha hao wawili waliotimuliwa Azam, kwa pamoja wamewahi kuwa walimu wa klabu ya Yanga na walijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu, Pluijm akitokea Singida United na Mwambusi akiwa huru.