Mbappe wa kwanza kuwasili kambini PSG

0
275

Nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe amewasili mapema zaidi kwenye kambi ya klabu yake ya PSG kulinganisha na wachezaji wengine wa klabu hiyo waliokuwa wakishiriki kombe la duni nchini Qatar.

Baada ya Mbappe kuwasili kambini nyota wa Morocco, Achraf Hakimi naye amewasili kwenye kambi ya klabu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu ya ufaransa l, League 1, inayorejea Jumatatu ijayo.

Hali ikiwa hivyo kwa nyota hao wawili ambao wamecheza mpaka hatu za mwisho za kombe la dunia nchini Qatar, Lionel Messi yeye bado anaendelea na shangwe akiwa nchini kwao Argentina.

Nyota mwingine wa PSG Neymar hajawalisi kambini licha ya timu yake ya taifa ya Brazil kuondolewa mapema katika hatua ya robo fainali ya kombe la dunia lililomalizika mwishoni mwa wiki kwa Argentina kuibuka mabingwa.